Thursday, May 3, 2012

Alice Foundation yawakumbuka watoto wanaoishi katika mazingira magumu na hatarishi kwa kuandaa hafla ya michezo na chakula cha mchana 26th april 2012

Hafla  ya michezo pamoja na watoto wanaoishi katika mazingira magumu na hatarishi lengo hasa lilikuwa ni watoto waweze kupata haki yao ya michezo pamoja na kufahamiana na kubadilishana mawazo.watoto walikuwa zaidi ya 400 ambapo wapo wanaosoma shule za msingi na sekondari katika kata yetu ya ubungo watoto hao walishindana michezo mbalimbali ikiwemo mpira wa miguu, mbio za magunia, mbio za kupokezana vijiti, kukimbia na kijiko na yai, kuvuta kamba na maswali ya ufahamu wa afya na mazingira. baada ya mashindano washindi walipata zawadi mbalimbali yakiwemo mabegi ya shule, miswaki, madaftari,kalamu na nyinginezo.
baada ya mashindano ulikuwa ni wakati wa kunywa na kula.. katika watoto hao baadhi ni wale tunao wasomesha, wengine kulipiwa nauli za shule na kupata huduma nyingine za msingi kutoka Taasisi yetu ya Alice Foundation.







Taasisi ya Alice yenye makazi yao eneo la ubungo NHC (sinza legho kituo cha basi)jana iliandaa hafla kwa watoto waishio katika mazingira magumu waishio katika kata ya Ubungo ambapo pia iliwakutanisha watoto hao na wengine waliopo shuleni.

Akizungumza na Elimubora Mkurugenzi wa Alice Foundation , Ms. Alice James Dosi alisema kuwa hafla hiyo inalenga kuwaweka pamoja watoto waishio katika mazingira magumu kuwafariji na kuwapati ushauri nasaha.

Alisema kuwa watoto 400 walishiriki hafla hiyo iliyoshirikisha michezo mbalimbali kama vile kuvuta kamba, mbio za mayai katika kijiko, kunywa soda, kupokezana vijiti, kukimbia na magunia.

Alisema kuwa watoto walifurahia tukio hilo na alisisitiza kuwa litakuwa likifanyika mara kwa mara.

Taasisi hiyo ya Alice inajishughulisha pia na masuala ya utunzaji wa mazingira, uwezeshaji wa akina mama, haki za wanawake, kusaidia watoto waishio mazingira magumu na  masuala ya Mkukuta.

No comments:

Post a Comment