Thursday, May 3, 2012

Alice Foundation yawakumbuka watoto wanaoishi katika mazingira magumu na hatarishi kwa kuandaa hafla ya michezo na chakula cha mchana 26th april 2012

Hafla  ya michezo pamoja na watoto wanaoishi katika mazingira magumu na hatarishi lengo hasa lilikuwa ni watoto waweze kupata haki yao ya michezo pamoja na kufahamiana na kubadilishana mawazo.watoto walikuwa zaidi ya 400 ambapo wapo wanaosoma shule za msingi na sekondari katika kata yetu ya ubungo watoto hao walishindana michezo mbalimbali ikiwemo mpira wa miguu, mbio za magunia, mbio za kupokezana vijiti, kukimbia na kijiko na yai, kuvuta kamba na maswali ya ufahamu wa afya na mazingira. baada ya mashindano washindi walipata zawadi mbalimbali yakiwemo mabegi ya shule, miswaki, madaftari,kalamu na nyinginezo.
baada ya mashindano ulikuwa ni wakati wa kunywa na kula.. katika watoto hao baadhi ni wale tunao wasomesha, wengine kulipiwa nauli za shule na kupata huduma nyingine za msingi kutoka Taasisi yetu ya Alice Foundation.







Taasisi ya Alice yenye makazi yao eneo la ubungo NHC (sinza legho kituo cha basi)jana iliandaa hafla kwa watoto waishio katika mazingira magumu waishio katika kata ya Ubungo ambapo pia iliwakutanisha watoto hao na wengine waliopo shuleni.

Akizungumza na Elimubora Mkurugenzi wa Alice Foundation , Ms. Alice James Dosi alisema kuwa hafla hiyo inalenga kuwaweka pamoja watoto waishio katika mazingira magumu kuwafariji na kuwapati ushauri nasaha.

Alisema kuwa watoto 400 walishiriki hafla hiyo iliyoshirikisha michezo mbalimbali kama vile kuvuta kamba, mbio za mayai katika kijiko, kunywa soda, kupokezana vijiti, kukimbia na magunia.

Alisema kuwa watoto walifurahia tukio hilo na alisisitiza kuwa litakuwa likifanyika mara kwa mara.

Taasisi hiyo ya Alice inajishughulisha pia na masuala ya utunzaji wa mazingira, uwezeshaji wa akina mama, haki za wanawake, kusaidia watoto waishio mazingira magumu na  masuala ya Mkukuta.

Alice Foundation ikishirikiana na ofisi ya serikali ya mtaa Ubungo NHC na jeshi la polisi yaandaa mkutano wa wazi na wananchi kwa legho la kuelimishana umuhimu wa polisi jamii na ulinzi shirikishi

ACP Kiondo na Mwenyekiti na mwanzilishi wa Alice Foundation wakati wa mkutano na wananchi juu ya polisi jamii na ulinzi shirikishi

 wananchi wakisikiliza kwa makini wakati mgeni rasmi ACP kiyondo akihutubia juu ya polisi jamii na ulinzi shirikishi
 Mkuu wa kituo cha polisi Urafiki Afande Paparika na mwenyekiti wa Alice Foundation Ambaye pia ni mkurugenzi wa Alice Fashion World na Founder wa Alice Foundation  Ms. Alice James Dosi kushoto ni Mr. Chillo Bunto Volunteer wa Alice Foundation
 Afisa mtendaji kushoto akifuatilia kwa makini mafunzo kutoka kwa ACP Kiondo
 wananchi wakisikiliza kwa makini wakati mgeni rasmi ACP kiyondo akihutubia juu ya polisi jamii na ulinzi shirikishi
polisi jamii katika kata yetu ya Ubungo

8th march international women's day, lauch of stop gender based violance- Alice Foundation

 maandamano ya amani katika uzinduzi wa kampeni ya kupiga vita unyanyasaji wa kijinsia- hafla zilizoandaliwa na Alice Foundation

  maandamano ya amani katika uzinduzi wa kampeni ya kupiga vita unyanyasaji wa kijinsia- hafla zilizoandaliwa na Alice Foundation
 Mwenyekiti na mwanzilishi  wa Alice Foundation ambae pia ni mkurugenzi wa Alice Fashion World akimwelekeza jambo mgeni rasmi ambaye ni Mbunge  wa jimbo la Ubungo Mh. John mnyika katika uzinduzi rasmi wa kupiga vita unyanyasaji wa kijinsia machi 8 2012 katika viwanja vya sanaa jijini Dar.

wamama wakichangia wamazo katika uzinduzi wa kampeni ya kupiga vita unyanyasaji wa kijinsia.